Thursday, June 4, 2009

Je nchi yetu itaendelea kwa kutegemea misaada ya wageni na mataifa makubwa ya ulaya na marekani?

Waswahili husema mtegemea cha ndugu hufa masikini. Kauli hii inafanana na hali inayoendelea sasa katika nchi nyingi barani afrika ambapo serikali kutwa kiguu na njia na kopo la kuomba msaada hasa katika mataifa yaliyoendelea na mabenki makubwa ya dunia. Je hii ni njia bora ya kutatua ama kukuza uchumi wa nchi hizi?

1 comment:

Anonymous said...

Uchumi wa nchi hauwezi kukua kwa kutegemea misaada kutoka nchi za nje moja kwa moja kwani msaada humfanya mtu awe na uwezo mdogo wa kufikiri namna ya kutatua matatizo.
Ukitaka kuifanya nchi iweze kukua kiuchumi inabidi wananchi ni lazima watambue wajibu wao pamoja na kuwa na viongozi wenye kujali maslahi ya wananchi wake.