
Hii ndio sababu wazotete imeamua kuweka mada zinazohusu jinsia na wanawake ili kuweza kuibua mijadala iliyofichika baina ya wanafunzi na hivyo kuonya jamii juu ya athari zake kwa vizazi vijavyo. Mada ya wiki hii: "Uwepo wa nafasi za upendeleo kwa wanawake ni njia pekee ya kueleta usawa wa kijinsia katika jamii ya kitanzania".
Shule zitakazo pambana ni Shule ya sekondari ya Baptist ambao watakubaliana na mada hii, pia watawakilisha Wizara ya maendeleo ya jamii, wanawake, jinsia na watoto na wapinzani wao watakuwa Shule ya sekondari ya Green Acre ambao wataka watakilisha Mashirika yasiyo ya kiserikali na watapingana na mada hii. Usikose kuangalia mfululizo wa vipindi hivi katika luninga yako ya TBC -1 kuanzia saa 10.05 jumapili na marudio yake ijumaa muda huo huo.
No comments:
Post a Comment