Wednesday, March 4, 2009

Baptist wala za mnato ndani ya wazotete

Waandazi kama kawaida wakipata mawili matatu kabla ya mchuano wa wazotete kuanza ndani ya ukumbi wa British council.

Nae ndugu yetu Balozi hakuwa nyuma kwenye orientation ya wanafunzi...




Vijana kutoka shule ya sekondari Baptist wakipozi kwa picha za mnato baada ya shughuli pevu ya kujadili mada na kujibu maswali mazito katika kipindi cha wazotete. Kama kawaida mdau faraji alijumuika katika kihafla hicho cha kupata kumbukumbu.

2 comments:

Anonymous said...

Kwanza nawapongeza waendeshaji wa kipindi cha wazo tete, majaji na vijana wanao jitokeza kushiriki mada!

Mimi kama mdau wa maendeleo ya vijana nafurahishwa na kipindi hiki ambacho kinaamsha ari za vijana katika kutafuta maarifa.

Mada iliyojadiliwa na vijana wa baptist na green acres kuhusu jisia ni mada nzuri ambayo vijana wanapaswa kujua, ingawa maoni yangu yageegemea upande wa wanaopinga mada! Wanawake ni kundi mojawapo maalum kwenye jamii kama lilivyo kundi la watoto au vijana kwahiyo halipaswi kushikiwa bango peke yake katika kutafuta uwakilishi katika vyombo vya maamuzi, vijana pia ni kundi muhimu ambalo uwakilishi wake kwenye vyombo vya maamuzi ni muhimu sana lakini hautiliwi maanani, kwa mfano uwakilishi wa wanawake ni zaidi yaasilimia 30 sasa kwenye bunge, lakini uwakilishi wa vijana ni chini ya asilimia 1, na asilimia takribani 67 ya nguvu kazi ya taifa ni vijana lakini hawana uwakilishi katika ngazi za maamuzi. Kwahiyo nalileta hili wazo tete kwenu waandaaji wa hiki kipindi muone ni namna gani mnaweza kuwafanya vijana wakaona huu upande unaosahaulika!

Naitwa
Mathias
Arusha

Tembelea web/blog hii: http://www.allianceforchildrenandyouths.webs.com/

wazotete said...

Ahsante bwana mathias kwa mchango wako muhimu.

wazotete