Monday, March 30, 2009

Je umaskini ni chanzo cha Rushwa nchini?

Usikose kufuatilia mfululizo wa kipindi hiki cha wazotete katika luninga yako uipendayo inyokuletea habari za ukweli na uhakika TBC1 kila jumapili na marudio ijumaa saa 10.05 jioni. Shule za sekondari za Ugombolwa, Kinyerezi, Migombani, Pugu, Kivule na DSM ndizo zitatuendeshea mjadala huu muhimu kwa taifa letu.
Katika mjadala huu, Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) watashirikiana na waandaaji wa kipindi hiki ambapo shule sita zitapewa wahusika na kutakiwa kuzungumza kwa niaba yao namna wanavyohusika na vita dhidi ya rushwa.
wahusika wetu: Daktari, Mwalimu na Mwanasiasa ambao watakubaliana na mada wakati Mwekezaji, Mfanyabiashara na Mkulima watapinga mada hii.

No comments: