Saturday, March 21, 2009

Habari mpasuka: Ridhwaa wagoma kushiriki wazotete...mkuru adai maadili hayawaruhusu!

Katika hali isiyo ya kawaida shule ya seminari ya kiislamu ya Ridhwaa, imekacha kushiriki kipindi cha wazotete wiki hii kwa kile walichokiita kulinda maadili ya kiislam kutokana na mada husika kuwa na mapungufu kimantiki.
Wakihojiwa na mtayarishaji wa kipindi hiki kwa njia ya simu, uongozi wa ridhwaa wamesisitiza hoja hiyo ambayo kwa mujibu wa mafundisho na maandiko hasa kitabu kitakatifu cha Quran katika sura ya 17 imeeleza bayana kuwa waislam hawapaswi kuikaribia zinaa. Na kutokana na maandiko hayo hawangekua tayari kuwaachia wanafunzi waende kuzungumzia masuala hayo.
Hata hivyo, walipohojiwa zaidi kuhusu uhusiano wa mjadala na kukaribia tendo hilo, mwalimu mhusika (jina kapuni) aliweka wazi kuwa uwezo wa wanafunzi wake ni mdogo na hawangeweza kuchambua mada hiyo vizuri huku akitolea mfano wanafunzi walioshiriki mjadala wa siasa ya ujamaa kuwa hawakuweza kuichambua ipasavyo na kupotosha maana mzima ya kipindi hicho.
Pamoja na maelezo hayo, sisi kama waandaji wa kipindi hiki tumeamua kuendelea na mjadala wetu na tutawashirikisha wajuzi wa masuala ya imani ili waweze kutupa ufafanuzi wa jambo hilo kwani tunaamani kuwa uongozi wa shule hiyo hawaja watendea haki wanafunzi wao kwani hii ilikuwa nafasi muhimu kwao kutoa maoni yao kuhusu elimu wanayoipata shule hapo....na kujitoa kwao kumeibua hisia tofauti za aina ya vijana tunaowaandaa kwa taifa la baadae.
Mada: Maendeleo ya sayansi na Teknolojia yamechangia kuongozeka kwa vitendo vya ngono zembe miongoni mwa vijana
Shule: St. Mary Secondary school v/s Ridhwaa Islamic seminary
Balloon: St. Mary Secondary School (Vyombo vya Habari) na Ridhwaa Islamic Seminary (Asasi zisizo za kiserikali).
Kwa taarifa zaidi: Usikose kutazama TBC-1 siku ya jumapili saa 10.05 jioni na marudio ijumaa saa 10.05 jioni....

124 comments:

wazotete said...

Matumizi mabaya ya sayansi na teknolojia ndio yanasabisha upotevu wa maadili na vijana wengi kufanya ngono zembe. Hassan Simba, wa Mbagala Charambe

wazotete said...

Matumizi mabaya ya sayansi na teknolojia ndio yanasabisha upotevu wa maadili na vijana wengi kufanya ngono zembe. Hassan Simba, wa Mbagala Charambe

wazotete said...

Matumizi mabaya ya sayansi na teknolojia ndio yanasabisha upotevu wa maadili na vijana wengi kufanya ngono zembe.

wazotete said...

Jamani tunawaombeni sana mfike shule za mikowani,hamtutendei haki kabsa. Naitwa Leonard Allen, wa Tabora Isevya.

wazotete said...

Munachangia ukimwi kuenea ndio maana hata rais mwinyi alichapwa kofi kwa hutuba zake zakikondom.Mnakera sana!

wazotete said...

Naitwa mwl Geofrey kilowoko wa mbeya. Uongozi wa shule ya Ridhiwaa hawaelewi tofauti ya dini na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Tunamshukuru shehe kwa elimu

wazotete said...

Ninge penda mshirikishe shulembalimbali naitwa diana wa dom

wazotete said...

NEEMA SAYANSI NATEKNLJ INACHANGIA KIASI KIKUBWA SANA .TABORA.

wazotete said...

Sayansi na teknology imesaidia sana ngono zembe ni tabia ya mtu mwenyewe (mafanikio yameletwa na sayansi na tekn) mama alliy ngaramtoni arusha

wazotete said...

Science na tech imechangia kueneza ukimwi kwani hata utengenezaji wa kondom ni hayo wakati kondom si kinga kamili.MR NICO WA MWANZA

wazotete said...

NAITWA ELISHA WA MWANZA MIMI NAWAUNGAMUKONO SENTIMELIZI

wazotete said...

KIV WANATISHA INAONYESHA WAMEPKWA VZR NA WLM WAO NA NIWA2 WANAOZNGATIA.ALSON MWANGWALE MBZ MWSHO D'SALAAM

wazotete said...

Kipindi kimetulia,nawashauri wanafunzi wakiangalie mi Amina Haidhuru

wazotete said...

HIKI KIPINDI NIKIZURI ILA TUNAOMBA MSHIRIKISHE NA SHULE NYINGINF ZA NJE YA DAR. TZ SIO DAR TU

wazotete said...

Si kweli kwamba science na tech inachangia kufanya machafu isipokua kwa wale wasiokua na maadili ya dini

wazotete said...

mimi naitwa enoth nipo arusha nakubali sayansi na technologia inachangia kuwepo kuwepo kwa ngono zembe

wazotete said...

NaitwaLinusMpembanipoS'wangaViongoziwashulewaliozuiawanafunzikushilikinimakosakwanyakatizaUwazinaukwelisivema

wazotete said...

NAITWA MNONGORA WA TMK MAJARIDA MENGINE YANACHANGIA NGONO KWANI PICHA NYINGI ZICHAPISHWAZO ZINAPOTOSHA SANA!+<20>

wazotete said...

Ngono ni roho. Ni msukumo. Kuishinda inatakiwa Roho nyingine. Ngono ilikuwepo kabla ya teknolojia. Ni swala la mtu binafsi. Teknoloj haihusiki hapo. Mama Ben.

wazotete said...

Ibrahim Matiti wa Mbeya.Hao viongoz wa Ridhwaa wakapimwe akili maana hil janga ni la taifa zima bila kujal dini,mila na destuli wala siasa!!

wazotete said...

Je nikweli mikoa ya pwani wanapo wa weka mabinti ndani huwafundisha kuishi nawanaumetu ? Ibra nipo Tabata riwith

wazotete said...

Napenda kuwapa big up kruu nzima inayo endesha kipindi cha wazo tete.I'm Hezbon Namwel from Mara, musoma.

wazotete said...

napenda kuwasahihi uongozi wa hiyo shule je? Hawapendi tushee idea katika kutokomeza magonjwa yanayosababishwa na ngono zembe mimy mkereketwa .ANGEL

wazotete said...

SERIKARI AU VYOMBO VYA HABARI VIANGALIE MAMBO YA KUIJENGA JAMII SIO KILA JAMBO LINAFAA KWA JAMII. NI GIBSON JACK KUTOKA UYOLE/MBEYA. AHSANTE.

wazotete said...

Nimesikitika na hao walimu waliozuia wanafunzi wao,kama mzazi nilitarajia walimu ni wazazi wa pili kufundisha watoto,hongera kivule kushiri.Dorkas Nkembo Moshi

wazotete said...

Naitwa MACKA MARWA wa Nyamongo(TARIME) napenda kuwapongeza sana kwa kuleta mada hii ya sayansi na teknolojia kwani inahusu sana vijana wa kizazi hiki.

wazotete said...

Sayanc na technology ndio chanzo cha ngono uzembe. Kwa njia za Tv mfano picha za X kwenye magazeti yanayo husika na mapenzi. Kwa jina Zaina Kagunia kutoka Moshi

wazotete said...

Naitwa saidi au kurwa kutoka singida samaki ameshajikunja na ame kauka nusu nusu mbichi sayansi / tekinolojia imekolea utama/ dini imezidiwa imebaki imani tu.!

wazotete said...

Mimi Carlos wa Migo*2 napinga kuwa syns na tknlga huchangia kuenea kwa ngono zembe,mbona kuna baadhi ya makabila hutumia mila zao kufunda wali mf. Mafiga 3.Why?

wazotete said...

Ukafili ni ukafili tu juwa uasharati utawaangamizeni hata mjadili vipi na ukimwi hauuwi kama malelia yusufu nipo tabora

wazotete said...

NAITWA CHANDE NASORO NIPO DAR MIMI BINAFSI NAKUBALI KWAMBA KUKUA KWA SC NA TK CHANZO CHA NGONO ZEMBE.

wazotete said...

David lackson airport dsm,science & technology inachangia somehow cuz most of us ni wa2 wakukopi vi2 bila kujua athari zake.

wazotete said...

Vjana wa cku hzi 2ona kuw kufanya ngno ni fashion.hatuzingatii athali tutakazopta baadae.Naitwa Sheky naishi Tanga.

wazotete said...

NAITWA HADIJA MUDY NASOMA GREENBIRD GIRLS NAPENDA KUCHANGIA KWAMBA SAYANC NA TECKNOLOJIA INAJENGA HAIBOMOI HASA KUPATA HABARI MBALIMBALI NA MAFNZO NDANI MAIGIZO

wazotete said...

SALUMU.SAIDI.NATOKA..KIGAMBONI..NASEMA.SAYASI,.INAONGEZA..NGONO. UZEMBE

wazotete said...

hiyo sayansi inachangia ngono zembe tamaduni zipo toka zamani mbona ngono zembe azikuwepo sayansi natekerenojia imezidisha naitwa mama raya wayombo

wazotete said...

Wazoragu wasichana wanababisha gonozebe mimi ni martin

wazotete said...

SCIENCE AND TECHNOGY NI SHETANI,SI NGONO ZEMBE AU NGONO SALAMA VYOTE NI SHETANI KWANI KUJIKINGA NA HAYO MNAYOJADILI NI KUMRUDIA MUNGU.SHADRACK MWENDA, MTONI.

wazotete said...

mimi naitwa enoth nipo arusha nakubali sayansi na technologia inachangia kuwepo kuwepo kwa ngono zembe

wazotete said...

Binafsi siungi mkono hoja,sababu kuna vijiji vingi havina maendeleo na watu hawajui mitindo wala televishen.Ngono zembe ipo.BWENJE wa ARUSHA.

wazotete said...

NAITWA ATHUMAN ISSA NKWAMA NIPO IRINGA MAADA YA KWANZA NIMEIPENDA ILA NINGEPENDA KUWASHAURI WANAFUNZI NA VIJANA WENZANGU WAWEZE KUSHILIKI KTK VIPINDI HIVI

wazotete said...

Naitwa Aristides wa Manyara sayansi na Teknolojia kuenea gonjwa la ukimwi kwa kuangalia kwenye utandawazi .(Internet)

wazotete said...

Kiukwel sc&tech inachangia vijana kujikita ktk vitendo vya ngono zembe,ezi hukuti ki jana kajingiza ktk uchafu,vijana weng wana penda kujing iza tendo kimolo

wazotete said...

Sayansi na Teknolojia inachangia sana ngono uzembe.Mi Mwl. ANTON RWIZA kutoka mafumbo Kashai BUKOBA.

wazotete said...

Sayansi na Teknolojia inachangia sana ngono zembe.Mimi Musa Bau nipo Mtwara.

wazotete said...

Ellen wa mwanza naunga mkono point ya Ellen wa st.Mary.

wazotete said...

Naitwa mwl Geofrey kilowoko wa mbeya. Uongozi wa shule ya Ridhiwaa hawaelewi tofauti ya dini na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Tunamshukuru shehe kwa elimu

wazotete said...

NAITWA GRACE KANYANKOLE KUTOKA KARAGWE.MI NASEMA KUWA MAENDELEO YA SCIENCE NA TEKNOLOJIA IMESAIDIA KUPUNGUZA NGONO ZEMBE. p

wazotete said...

Naitwa Haule Kuzombe, Wanafunz ambo hawajafika wamekosea vby, je mada hii ikitolewa kwenye mtihani wa taifa, hawatalijadili?bado hawajaelimika.

wazotete said...

Naitwa victor ktk tabata Dsm,nakubaliana na mada kukua kwa sayansi na teknolojia kumesababisha vitendo vya ngono kuendelea kwa kasi.

wazotete said...

Mimi shafii kutoka Arusha wazo langu ninaona sayans inachangia ngono zembe

wazotete said...

NAITWA IBRAHIM NJOGOPA KUHUSU KUJITOA KWA HIYO SHULE MIMI NAONA SAWA LABDA MCHEPUO WA SHULE YAO AIRUHUSU.

wazotete said...

Naitwa Ali Nassor Ali ni mwanafunzi UDSM.Wanafunzi wa Ridhwaa kukataa kushiriki ni sawa kwani ngono ni ngono tu na hakuna ngono bila ndoa halali kidini.

wazotete said...

Mimi thabit nakubaliana na mtandao na mada ya ngono zembe lakini kuna nazaria na vitendo ss tuonesheni kwa vitendo ngono zembe mada hiyo inashinda hataunyago

wazotete said...

Naitwa afande mfuko wa singida sayansi na teknorojia haishawishi ngono zembe ila tunaitumiavibaya

wazotete said...

Naitwa soudy wa NUR ISLAMIC SEMINARY maendeleo ya sayansi na teknolojia ni kweli yanachangia ngono zembe ,kutokataa kwa RIDHIWAA kushiliki sijajisikia vizuri

wazotete said...

Asalam aley kum.kwa kuwa Ridhiwaa ni shule ya kiislamu nilitegemea wataonyesha upinzani mzuri hawakufanya jmbo zuri.Naitwa yahaya juma wa Arusha.

wazotete said...

Technology hasa media,yanachangia ngöno zembe.lakini pia jamii lezi imekuwa dhaifu ktk kuwajengea vijana utashi dhabiti na dhamira hai.

wazotete said...

naitwa rajabu naomba huyo ustadhi atuweke wazi kuhusu sayansi na dini yetu ya kiislamu inasema nini kuhusu swala hilo

wazotete said...

Prof. Verdiana Masanja Rwanda. Unyago na jando anbazo ni mila zetu huchochea ufska kuliko S&T. Mikusanyiko ya kuchezwa ngoma ufuska balaa.

wazotete said...

Kweli sayansi na teknolojia imesababisha ngono coz vyombo vya habari vinaelekeza ngono kwa vijana wanasema wa2mie kondom!naitwa suzy turu.mbeya.

wazotete said...

Ridwaa islamic wapo sahihi. Uislamu unafundisha kuwa makini kwenye maongezi. Hapo mnahamasisha hamfundishi na ndio maana maneno mnay

wazotete said...

Sayansi na tech nolg inasababisha Ngono zembe kwa sbb watoto hutazama picha za ngono.Mimi HASAN MTOLA WA MBAGALA

wazotete said...

Mie naitwa Mama Amina niko ilala walichofanya lidhuwaa siyo kizuri wajirekebishe.

wazotete said...

Kivule ni wazuri sana tu ila majaji msibweteke na jina la St Marys. Jonas kutoka St john's of Tanzania Dodoma

wazotete said...

A.alykum msiizinishe ngono kwa majina ya kificho zembe sayansi na teknolojia vina msaada kwa maendeleo ya binadamu wala hausiani na ngono khalef sumbawanga

wazotete said...

naitwa rajabu naomba huyo ustadhi atuweke wazi kuhusu sayansi na dini yetu ya kiislamu inasema nini kuhusu swala hilo

wazotete said...

Mimi ATONY RWIZA toka Bukoba mafumbo Kashai.N ikweli utandawazi unachangia ngono uzembe.

wazotete said...

Hi...! Sir. RHINO WA SBA, MAENDELEO YA SAYANSI NATEKNOLOJIA YANACHANGIA KWA KIAC KIKUBWA UKIZINGATIA KUMBIZA STAREHE WAKISHIKANASHIKANA WANANOGEWA........!

wazotete said...

Ridwaa si woga kama munavyofikiria bali wanamuhofia mola wao.amina ahmed wa m.yanga tandika

wazotete said...

MUWAALIKE NA BRAGHT ANGEL ILIYOKO MKULANGA,ONGELENI KWA KIPINDI KIZURI BY BALOLE.

wazotete said...

SAYANSI NA TEKENOLOGIA IMECHANGIA SANA HOW SURE I,U THAT CONDOM IS 100%.BOMERA FRM ARUSHA

wazotete said...

NAITWA ELINA WA KIGAMBONI MIMI NAONA KUJIHUSISHA KATIKA NGONO ZEMBE NI AKILI YA MTU MWENYEWE,NI HAYO TU

SALUM MSANGULE WA KILOSA SAYANSI NA TEKNOLOJIA AICHANGII NGONO ZEMBE

wazotete said...

Naitwa Ernest nipo Kiwira MBY,Ukweli hakuna baya ilasi busara kuwalaum wanafunzi kwani wao pia wanawamiliki wao(ADMINSTRATION)Ubaya haupo zaidi yakutiadoa Uislm

wazotete said...

Naitwa mariam yakub wa meli 4 zenji kwa muisla akuna ngono zembe wa salama subiri ndoa

wazotete said...

naitwa ali hamad wa tandika dsm nachangia mada kwamba sayans na teknologia inachangia ngono zembe kwa vijana

wazotete said...

Kila kitu kina faida na hasara,na kwasasa tunaangalia kitu cha faida,hatuwezi kufanya kitua chenye maana cha jamii ijiangalie yenyewe by BINJUMAA & ZENA TABORA

wazotete said...

Napenda kuchangia hoja. Sayansi na teknoloji yamepunguza kwa asilimia kubwa ngono zembe. Na hy ni tabia ya mtu. Anna wa mbinga

wazotete said...

Naitwa grace kutoka dom.msisingizie sayansi na teknolojia zembe ngono ni tabia ya mtu
P.mbiro

wazotete said...

Naitwa Isaac Marwa wa KEMORAMBA SECONDARI Musoma,maendele ya sayansi na technic yanachangia,vi2kama picha zaX zinachangia kuwepo kwa ngono zembe.

wazotete said...

Naitwa maua wa sumbawanga sayansi na teknolojia yanachangia kuepusha ngono zembe maana vitu vyote viko wazi

wazotete said...

Naitwa OSCAR NZIKU niko Mbeya kwakweli shule iliyo jitoa jalibuni kuuelimisha utawala wa shule hiyo kwani mada ya leo ni yakuelimishana vijana.

wazotete said...

Naitwa akongwa venance nipo Manow High school Tukuyu nawapa big up waandaaji wote wakipindi hiki maoni yangu m2tembelee nasisi wa mbeya 2weze kutoa mawazo ye2.

wazotete said...

Enz 2lizopo sasa ni enz za saut nying, nienz za kelele hivyo bac vijana wanapaswa kupambanua saut hz nakufwata inayofaa @ DG

wazotete said...

Hiyo shule imekosea kuwakataza wanafunzi kuja kushiri ingekataza wanafunzi wote waislam wasishiriki sababu mbona wanafunzi ambao wako st mary's wameshiriki.

wazotete said...

Zaman hakuwepo sasa yapo kilajambo nawakati hundiyo wakat wake

wazotete said...

Ridhiwaa wangekuja tu,watoe dukuduku lao from moshi.

wazotete said...

Ridhiwaa hawana kosa ndio wanao nesha msisitizo( sayansi na teknolojia inachangia ngono zembe kwa vijana. Mama salahi znz .

wazotete said...

mimi maoni yangu ni hiyo shule ni ya dini siyo ya kawaida je hawafundishwi,kujikinga,ukimwi?inasikitisha,sana.Ramagudy SGD.

wazotete said...

NAITWA JOHN MAKUNGA WA MBEYA NGONO ZEMBE HASA NA POMBE ZINA CHANGIA SANA WALA SIO SAYANSI NA TECKELONIJIO

wazotete said...

SAYANSI NA TEKNOROJIA INACHANGIA SANA NGONO, KWASABABU MAMBO MENGI 2 IKIWEMO INTANET NA CM ZIMERAHISISHA KABISA NAITWA MNONGORA WA TMK.!+<20>

wazotete said...

NICK NYOVE WA IRINGA KWA UJUMLA WALIMU WAMEKOSEA SANA KWANI WAMEWANYIMA HAKI ZAO ZA MSINGI

wazotete said...

Sayansi na Technolojia imeharibu jamii. Na malezi mabaya ya Famili zinajidai za kizungu.

wazotete said...

Naitwa Bonita pascali.Napinga kabisa hiyo mada kuna msemo unasema Abilia chunga mzigo wako.Bila sayansi naTeknolg tungefika wapi?

wazotete said...

NAITWA MTEMI KANGALOO MIMI NAONA TATIZO KUBWA LINALO CHANGI NGONO UZEMBE NI ULEVI NA MAVAZI YA AKINA DADA

wazotete said...

S/technology haichangii ngono zembe,condom zimetoka wapi?,kwani enzi za kale hapakua na ngono zembe?,hakuna kusingizia technlgy.lweganwa john SAUT MZA

wazotete said...

Naitwa Astilda mugolozi wa kilombero mim4 napenda kusema kwamba sayansi na technolojia imesaidia kupunguza ngono zembe.

wazotete said...

NYIE..HAMWOGOPI..?.KAMA..MWINYI..ALIPIGWA.,KIBAO.JE.NINYI.HAMTACHINJWA?.KABISA.NA.WAJAHIDINA.KWA.HOJA.HIYO.YA.NGONO.UZEMBE,

wazotete said...

Miye Obeline Moshi Mbulu.KUKUA kwa sayansi na teknolojia haichochei ngono zembe bali watu wenyewe kukosa maadili. MADA HIYO INAELISHA JAMII

wazotete said...

MAENDELEO YA SYS NA TKNJ HAYA SABABISH ILANI KUIGA TAMADUNI ZAKGENI NDIO CHACHU YANGONO ZEMBE,VENANC GASPAR IPL TABORA

wazotete said...

Naitwa Hafsa wa Martin Luther,Dodoma. Maendeleo ya sayansi yanachangia uwepo wa ngono zembe kutokana na mabadiliko ya tamaduni.

wazotete said...

Naitwa mwl Dulla nipo mpanda sayansi na teknolojia haichangii ngono zembe bali ni tabia ya mtu

wazotete said...

Naitwa Israel mwakilasa wa kilombero-Ruaha.sayns na teknj inasaidia kupungunza kuendelea na ngono zembe kwani tunaona jinsi watu wanavyopoteza maisha.

wazotete said...

HAYO MAENDELEO YENU YA SAYANSI NDIO YAMECHANGIA BALA KUBWA LA NGONO ZEMBE KUPITIA SAYANSI MI NASEMA SAYANSI IMECHANGIA MI HAWA DAR.

wazotete said...

Ridhiwaa wangekuja tu,watoe dukuduku lao from moshi.

wazotete said...

Acheni kulaum shule iliyogoma kushiriki.Wamefuata sheria hasa.Dini ya Kiislam haiendeshwi na mawazo ya watu.NI SHERIA YA MUNGU,na ni lazi kuifuata.By Mhd Kombo.

wazotete said...

Naitwa khadija sudi wa nyarugusu zanzibar,kweli sayansi na teklonojia inachangia sisi vijana kuharibika na kufanya ngono.

wazotete said...

Sayansi na Technolojia imeharibu jamii. Na malezi mabaya ya Famili zinajidai za kizungu.

wazotete said...

Naitwa Tausi wa tabata sayansi na teknolojia havichangii vijana kufanya ngono zembe,kwan ngono zembe ni tamaa ya mtu mwenyewe.

wazotete said...

naitwa wanda wa boko napenda kuwapongeza kwa kipindi kizuri pamoja na mada nzuri,

wazotete said...

Maendeleo ya Science/tech.yanachangia ngono uzembe bcoz through tv etc vijana wanashawishika.Mwl MATUGA wa Itule S.S.

wazotete said...

Sisi vijana tunapenda sana ngono zembe tumepotea mm almasi arusha unga limitedi.

wazotete said...

Maendeleo ya sayansi na tekn yanapunguza ngono zembe kwa sababu elimu inatolewa kwa njia mbali mbali hata katika madhehebu naitwa neema josephat Ngudu

wazotete said...

HOLLOW NAITWA SUBIRA WA DODOMA NA FAGILIA SANA KIPINDI CHA WAZO TETE KIZURI SANA KINA ELIMISHA TBC WAAAA BIG UP

wazotete said...

USIPO WAELIMISHA VIJANA NA KUWAPA MAADILI UTA WAELIMISHA WAZEE? HIVYO NA ULAUMU UONGOZI WA SHULE HIYO. NI REHEMA R. KUTOKA KARATU.

wazotete said...

Ni kweli sayans imeleta mafanikio lkn kwa kiasi kikubwa imevuruga mfumo we2 wa maisha kwa ujumla, sababu tunaiga sn, ngono live ktk tv! eddy khalef.

wazotete said...

MAENDELEO YA SAYANSI NA TECHNOLOGIA YANACHANGIA KUONGEZEKA KWA NGONO UZEMBE KUTOKANA MEDIA TOFAUTI KAMA TV NA HATA KATIKA ENTERNANT PAMOJA NA SIM.DONATA

wazotete said...

Ridhiwa wako right ,kwenye uislam hakuna ngono zembe , ngono ni ngono tu.maadili ya uislam hayaruhusu muislam kutetea ngono ya aina yeyote. Ramadhan from ZNZ.

wazotete said...

Jamani malezi ya wazazi wetu ndo yanachangia we mtoto atatoa wapi hela ya kununua vitu vya anasa? John Musiba wa Nansio ukerewe

wazotete said...

Kijana mwenyewe ndio chanzo cha ngono zembe sio sayansi na teknolojia,kwani yeye ndiyo anaamua aweje.JUDITH

wazotete said...

BUMI wa arusha ni kwel maendleo ya sayans na teknolojia yanasababishia kuwepo kwa ngono zembe.

wazotete said...

Mim ni koku nimefuraia sana maada ya leo nawapa big up waandaaji.

wazotete said...

HONGERA TBC 1 KWA KUTUELIMISHA KUPITIA VIPINDI VYENU KAMA WAZO TETE NI MIMI MAGORI WAMBURA from MUSOMA

Anonymous said...

Hey Hey, I am new to these parts. suppose make an introduction.

see you around and Thankyou

(sorry if this is the wrong place to put this post)